Friday, 11 May 2018

Baada ya mvua kuharibu miundombinu Dar, serikali kufanya tathmini

Serikali imekiri miundo mbinu kuharabika baada ya mvua nyingi kunyesha kwa jiji la Dar es salaam.
Akizungumza leo, Mei 11 Naibu Waziri TAMISEMI, Joseph Kandege amemuhakikishia Mbunge Abdallah Mtolea aliyehoji kuwa
Tatizo lililopo katika Jimbo la Segerea linafanana na lililopo katika Jimbo la Temeke ambapo katika Kata za Buza Kata za Tandika na Kata 14 Temeke barabara zimeharibika sana hasa baada ya mvua hizi, nilitaka kujua serikali ina mpango gani wa kwenda kuzikarabati barabara hizo za mitaa katika Kata hii angalau kwa kiwango cha Changarawe?
Aidha Serikali imesema kuwa watafanya thathmini ya uharibifu uliotokea katika jiji hilo ili kuchukua hatua za dharula.
“Ni ukweli usiopingika kwamba baada ya mvua kunyesha maeneo mengi miundombinu yake imeharibika na hasa kwa jiji la Dar es es salaam ambalo mvua zimenyesha nyingi sana naomba nimuhakikishie Mh. Mbunge kwa kufanya tathimini ya uharibifu uliotokea ili tuchukue hatua za dharula ili at least wananchi watumie barabara zikiwa na hali nzuri,’’ amesema Kandege.

No comments:

Post a Comment