Monday, 21 May 2018

Baada ya BET: Rayvanny afafanua ishu ya kubadili muziki ili kunasa tuzo nyingine

Msanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Rayvanny amesema hana muziki kwa ajili ya kushindania tuzo au kwenda kimataifa bali anafanya kwa ajili ya mashabiki wake.

Muimbaji huyo amesema baada ya kushinda tuzo ya BET watu walifikiri angebadili aina muziki wake lakini sivyo alivyo yeye.
“Watu walikuwa hawajaelewa, walikuwa wanafikiri tuzo zinafanana na muziki wa aina fulani lakini nyimbo zilizonifanya nichukue tuzo ni hizi hizi za nyumbani,” amesema.
“Hakuna nyimbo za kuchukulia tuzo, hizo za nyumbani, mimi nafanya muziki kwa ajili ya mashabiki zangu na watu wa Afrika Mashariki,” Rayvanny ameiambia Bongo5.
Utakumbuka June, 2018 Rayvanny alishinda tuzo ya BET 2017 katika kipengele cha International Viewers Choice.

No comments:

Post a comment