Wednesday, 30 May 2018

Asimamishwa kazi kwa kumuita ripota ‘Handsome’ wakiwa live


Waziri wa Habari nchini Kuwait amemsimamisha kazi mtangazaji wa habari wa  kituo cha Kuwait TV baada ya kumuita ‘ripota Handsome’ wakati walipokuwa mubashara kwenye kipindi.

Basima al-Shammar amekutana na kadhia hiyo wikiendi iliyopita wakati alipokuwa akitangaza uchaguzi wa manispaa nchini humo na ndipo alipomtania ripota ambaye alikuwa akijitengeneza  kabla ya kuanza kuripoti kuwa asijitengeneze sana kwani yeye ni ‘Handsome’ tayari huku wakiwa mubashara, kitu kilichotafsiriwa kwamba mtangazaji huyo alikuwa akijaribu kumtongoza ripota huyo.

Aidha katika utetezi wake Basima amesema kuwa katika shughuli za utangazaji ni utamaduni uliopo kumwambia mtu unaonekana vizuri (Handsome) ama uko poa kabla ya kwenda mubashara.

Hata hivyo waziri huyo ametupilia mbali utetezi wa mtangazaji Basima na kumsimamisha kazi huku akiamuru uchunguzi ufanyike kubaini kama mtangazji huyo alikuwa akijaribu kumtongoza ripota huyo.

No comments:

Post a comment