Wednesday, 2 May 2018

Alikiba atoa ahadi hii kwa mashabiki wake

Unatamani kuisikia ngoma mpya kutoka kwa Alikiba? Basi msanii huyo amahidi kufanya hivyo lakini kwa sharti moja tu.
Alikiba kupitia mtandao wake wa Instagram ameahidi kuachia ngoma mpya endapo video ya wimbo mpya wa Ommy Dimpoz aliomshirikisha Seyi Shay wa Nigeria ikivikisha views milioni 3
“Hii nyimbo Ya @ommydimpoz ikifika milioni 3 YOUTUBE Naliamsha DUDE 🤙🏾 (I PROMISE U) #SupportedByKiba #KingKiba,” ameandika Kiba.
Ngoma ya mwisho ya alikiba ilikuwa ni Seduce Me ambayo aliachia August 25, 2017 ukiachana na Maumivu Per Day ambayo aliachia Novemba 29 mwaka jana ambapo hata hivyo haikuwa rasmi.

No comments:

Post a Comment