Saturday, 21 April 2018

Zamaradi Mketemea Asimulia Alivyoumizwa na Kifo Cha Agness Masogange


Mtangazaji Maarufu wa Televisheni na redio, Zamaradi Mketemea amefunguka na kueleza alivyoguswa na msiba wa msanii Agnes Gerard Masogange aliyefariki dunia jana kwa matatizo ya pumu katika Kituo cha Huduma za Afya cha Mamama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Zamaradi amesema alimfahamu Masogange zaidi ya maisha yake ya kwenye mitandao ya kijamii huku akiweka wazi kwamba kuna kipindi Zamaradi alikwenda Afrika Kusini na kupokelewa na Masogange ambaye aliishi kwake kwa zaidi ya wiki moja, hivyo alikuwa kama mwanafamilia.

Mtangazaji huyo amesema amesikitishwa sana na kifo cha ghafla cha Masogange na kusema wamependekeza aagwe Leaders Club ili watu wengi wapate fursa ya kumuaga na kwamba atasafirishwa kwenda kuzikwa kwao, Mbeya.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: