Tuesday, 17 April 2018

YANGA YAENDELEA KUFANYA MAZUNGUMZO NA LWANDAMINA


Uongozi wa klabu ya Yanga umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha Kocha George Lwandamina anarejea kikosi hapo na kuungana na wenzake.

Taarifa za ndani zimeeleza, Yanga wamekuwa wakifanya juhudi hizo ili Lwandamina arejee na kujiunga na kikosi hicho na kukiongoza dhidi ya Wolayta Dicha.

"Kweli juhudi zinafanyika kwa kuwa kocha hakuwa amemaliza mkataba. Tunaona aje na kuungana na wachezaji atakapomaliza mkataba, basi anaweza kwenda ambako anakwenda.

"Tulianza mazungumzo naye baada ya kupata uhakika kuwa hakusaini mkataba na Zesco kama ilivyoelezwa. Wanatarajia kuasaini baadaye, hivyo si vibaya akaja kumalizia muda wake," kilieleza chanzo kutoka Awassa, Ethiopia.

Noel Mwandila ndiye ameridhi mikoba ya Lwandamina kwa muda. Tayari ameanza kazi ya kuinoa Yanga na kesho ina kibarua cha kuwavaa Wolayta Dicha wakiwa nyumbani.

Katika mechi ya kwanza, Yanga wakiwa nyumbani waliwanyoosha Wahabeshi hao kwa mabao 2-0.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: