Saturday, 7 April 2018

Yanga SC yawapa raha Watanzania Taifa


Kikosi cha klabu ya Yanga SC hii leo kimefanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya timu ya Welayta Dicha  ya nchini Ethiopia mchezo wa kombe la shirikisho uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
Waliyokuwa mwiba mkali kwenye ngome ya Waethiopia ni Raphael Daudi aliyefunga bao sekunde 30 tu tangu mpira kuwa na Emmanuel Martin aliepachika dakika ya 54 ya kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo wa nyumbani unaifanya klabu ya Yanga kuwa na matumaini ya kusonga mbele endapo watafanikiwa kulazimisha sare au kushinda mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Ethiopia

No comments:

Post a comment