Tuesday, 24 April 2018

Yanga kumpeleka kocha wao kesho kambini Morogoro

Yanga wanaonekana hawataki mchezo na Kocha wake mpya wa Yanga, Mwinyi Zahera tayari wamepanga kumepeleka mjini Morogoro, kesho.

Zahera amejiunga na Yanga leo na kutembezwa katika makao makuu ya klabu hiyo na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa yanga, Charles Boniface Mkwasa.

Kocha huyo raia wa DR Congo, anachukua nafasi ya Kocha George Lwandamina raia wa Zambia ambaye amerejea kwao Zambia na kujiunga Zesco.

Yanga ipo kambini Morogoro kujiandaa kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Zahera amefanya mazungumzo ya muda wa takribani saa moja na Mkwasa kabla ya kutembezwa sehemu kadhaa katika ofisi za klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment