Mabingwa wa soka nchini Tanzania Yanga SC wanatarajia kuondoka nchini Jumapili kwenda Hawassa Ethiopia tayari kwa mchezo wao wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Wolaita Dicha.

Yanga watakipiga na Wolaita Dicha Jumatano jioni kwenye Uwanja wa Hawassa mjini Hawassa. Klabu hiyo inaingia mchezoni ikiwa na mtaji baada ya kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Kitu cha tofauti kuelekea kwenye mchezo huo, Yanga hawatakuwa na kocha wao Mkuu, Mzambia, George Lwandamina aliyeondoka mapema Jumanne kwenda kukamilisha mipango ya kurejea kwenye klabu yake ya zamani Zesco United.

Kwa sasa benchi la Ufundi la Yanga lipo chini ya walimu watatu waliokuwa wasaidizi wa Lwandamila, Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazawa, Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: