Friday, 13 April 2018

Wolper: Siwezi Kusapoti Tena Kazi Za Harmonize


Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hataweza kukaa na kusapoti kazi za Harmonize sababu anamuonea huruma mpenzi wake Sarah.

Siku chache zilizopita Wolper alitengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye na mpenzi wa Harmonize Sarah kurushiana vita ya maneno kwenye Instagram.

Ambapo Sarah alimtaka Wolper aache kumtumia Meseji za kumtaka Mpenzi wake Harmonize jambo ambalo lilimkera Wolper kwani aliweka wazi kuwa akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa hivyo hakuwa yeye aliyekuwa anatuma Meseji.

Kwenye mahojiano aliyofanya leo na Sam Misago Wolper amesema kuwa ameamua kuacha kabisa kusapoti kazi za Harmonize:

'Mimi sio mswahili na wala sina uswahili tulianza mapenzi kwa mimi kusapoti kazi zako,` lakini sasa naona ili nisikwaze mahusiano yako naona bora nisisapoti kazi za Harmonize kwa sababu yule mwanamke wake anahitaji kuhurumiwa”.

Lakini pia Wolper amesisitiza kuwa amefikia uamuzi wa kumblock Harmonize na Sarah kwenye Instagram ili aepushe maneno maneno.

No comments:

Post a Comment