Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa Salma Jabu  maarufu kama Nisha Bebe hana vigezo vya kutembea na Ex boyfriend wake Brown.

Wiki iliyopita picha za Nisha na Brown zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wakiwa wanakumbatiana na hata kubusiana jambo lililozua maneno huku ikisemekana kuwa ni wapenzi.

Lakini mwishowe Nisha aliachia wimbo wake wa Bachela ambapo ilionekana kuwa Brown alikuwa ni video king Kwenye video hiyo na wawili hao baadae walikana tetesi zozote za Mahusiano ya kimapenzi wakidai ilikuwa ni kazi tu.

Hatimaye Wolper amefunguka kuhusiana na Mahusiano hayo na kuweka wazi kuwa haamini kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Wolper amedai kuwa Nisha ni mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo huyo na pia anazijua taype za wanawake wanaoweza kutembea na Brown haifanani kabisa na Nisha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: