Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo amezindua Jengo la kufundishia la ghorofa 10 katika Taasisi ya Teknolojia  Dar es salaam- DIT – Teaching Tower Complex.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua jengo hilo amesema kuzinduliwa kwa jengo hilo kutasaidia kuongeza udahili wa wanafunzi kwa kuwa jengo hilo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidia ya Mia Tisa kwa mara moja.

Ndalichako amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuondoa upungufu wa kero ya Miundombinu iliyokuwa inaikabili DIT kwa muda mrefu ambapo jengo hilo limeigharimu Serikali zaidi ya Bilioni Tisa ambazo ni fedha za ndani.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha DIT Profesa Preskedis Ndomba ameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo  uliofanywa na Serikali ambapo amemhakikishia Waziri wa Elimu kuwa  watailinda miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu kwa lengo la kuongeza tija ya kuwepo kwa wataalamu wa fani mbalimbali hapa nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
18/4/2018

Share To:

msumbanews

Post A Comment: