Suala la nyimbo za wasanii wa Bongo Flava kufungiwa bado lipo kwenye headlines za kiwango cha juu, safari hii mjadala mzima umeamia Bungeni mjini Dodoma.
Mjadala umeanzishwa na Mhe. Catherine Magige aliyeuliza ni kwanini kamati ya maudhui inaacha hadi wasanii wanatoa nyimbo ndipo inaibuka na kuzifungia bila kujali wasanii wanaangaika na kupitia changamoto mbali mbali hadi kuzikamilisha.
Akijibu swali hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kila taifa lina utamaduni wake na lazima liulinde, hivyo wanachokifanya sio vita na wasanii bali ni kulinda maadili katika kipindi hiki cha utandawazi.
“Tunachofanya hapa sio cha pekee duniani kila mtu anafanya hivyo, nitoe mfano mmoja mdogo, Rick Ross ambaye amepiga wimbo na Diamond ‘Waka’ amepata matatizo kwa kuimba wimbo ambao unaleta picha anaunga mkono ubakaji, wakina mama Marekani walikuja juu wimbo ukaondolewa kwenye TV zote na yule kijana akaomba radhi,” amesema Waziri Mwakyembe.
“Davido mwamuziki maarufu duniani ambaye amepiga na Diamond amefungiwa nyimbo zake mbili mwaka huu, sio huyo tu, Wizkid kafungiwa nyimbo zake, sijasikia wabunge wa Nigeria wakilalamikia sheria zao wenyewe,” amesisitiza Waziri Mwakyembe.
Ameogeza kuwa anashangazwa kwa wabunge kuhoji wao kufungia nyimbo chache wakati BBC katika historia yao wamefungia nyimbo nyimbo zipatazo 237.
February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: