Saturday, 21 April 2018

Waziri Mwakyembe amlilia Msanii wa bendi ya Mzee King Kiki


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa mwanamuziki wa dansi, Kalambay Bisongo aliyekua akifanya kazi kwenye bendi ya Wazeee Sugu ya Mzee King Kiki.

Bisongo alifariki April 18 ya mwaka huukatika Hospitali ya Mloganzila iliyopo maeneo ya Kibamba jijini Dra es Salaam. 

Msanii huyo amewahi kufanya kazi kwenye bendi tofauti tofauti ikiwemo Tanzania One, Achingo na baadae bendi ya King Kiki.

Soma taarifa hiyo ya Mhe. Mwakyembe hapa chini:
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: