Friday, 20 April 2018

Waziri Kalemani Asema Kingu ni Mbunge wa Mfano

Waziri wa Nishati Dr. Medard Kalemani Amewataka Wabunge kuiga mfano wa Mbunge wa Singida Magharibi kwa kuwa mbunge huyo ni lulu, mzalendo na mchapakazi, na hatulii katika kuhangaikia maendeleo ya wananchi wa Jimbo lake.

Dr.Kalemani Alisema hayo juzi wakati Akiwasha umeme wa backnorne katika kijiji cha Nkuninkana maeneo ha Utaho A
na Utaho B, sambamba na hapo aliwasha pia katika kijiji cha kingine cha  Isalanda maeneo ya Wibia,Msambu  katika Jimbo la Singida Magharibi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo  Mh: Kingu amezichangia kaya 160 kwa kuunganisha umeme pia Mh.Kingu alitoa fedha taslimu kwa kila kaya kuichangia Tsh. 5000  ( elfu tano ).

Wakati huohuo waziri Dr. Kalemani Alimuahidi Mbunge Kingu kusambaza umeme wa Rea phase 111 wiki hii katika vijiji vyote vya jimbo la Singida Magharibi ambapo kingu ni Mbunge wa Jimbo hilo.


Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: