Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Halmashauri zilizopata Hati Safi zimeongezeka  kutoka Halmashauri 81 kwa mwaka 2015/16 mpaka kufikia Halmashauri 166 (90%) kwa mwaka  2016/17.

Jafo ameyasema hayo wakati kwa Kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ukumbi Bunge kuhusu utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo ya CAG kwa hesabu za Mamlaka za Serikali  za Mitaa kwa  mwaka Ulioishia  Juni 30, 2017.

Alisema “napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa maelekezo yao mazuri yaliyosaidia sana utendaji kazi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na MSM; Michango yao, ushauri na maelekezo yamewezesha kuongeza Idadi ya Hati Safi.

Akizungumzia kuhusu hoja zilizobainishwa katika ropoti ya CAG Mhe. Jafo alisema tumefanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa katika ripoti zilizopita ambapo watumishi 434 wamechukuliwa hatua baada ya kubainika kusababishia halmashauri zao hasara/hoja zisizo za lazima kutokana na kutotekeleza ipasavyo wajibu wao ama kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu.

“Kati ya hao 9 wamefukuzwa kazi, Watumishi 210 wamepewa barua za onyo huku Watumishi 15 wakifikishwa kwenye vyombo vya dola. Watumishi 28 wamesimamishwa kazi, 13 wametakiwa kufidia hasara kutoka kwenye mishahara yao wengine 4 wameshushwa vyeo na wengine 10 wamebadilishiwa majukumu” alisema Jafo.

Aliongeza kuhusu MSM kupokea Fedha pungufu ya Bajeti Iliyoidhinishwa ni kwa sababu Serikali hutegemea makusanyo ya mapato kutoka vyanzo mbalimbali. Hivyo, kiasi kinachotumwa kwenye MSM hutegemea mwenendo wa mapato yaliyopatikana lakini pia fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa na Serikali kwa mwaka wa fedha uliotaguliwa 2016/17 zimeongezeka ikilinganishwa na mwaka  wa 2015/16.

Kwa  mwaka 2016/17 fedha za miradi ya maendeleo zilizopokelewa na MSM ni Tsh. 705,927,921,596.20 sawa na 57% ya bajeti iliyoidhinishwa ya Tsh. 1,242,616,839,000 akati mwaka 2015/16, fedha zilizopokelewa  zilikuwa ni Tsh. 390,525,992,297 sawa  39%  ya bajeti ya Tsh. 1,010,650,744,099.

Kuhusu changamoto katika Usimamizi wa Mapato katika Mhe. Jafo alieleza Wizara imeendelea kuziba mianya ya uvujaji wa mapato kwa kuhakikisha kuwa Halmashauri zinahamia katika matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ujulikanao kama Local Government Revenue Collection and Information System (LGRCIS) ambapo takwimu zote za mapato zinatunzwa katika mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mashine za kukusanyia mapato (Point of Sales) zinazotumiwa na Mawakala/Wakusanya mapato, na hivyo kuiwezesha Halmashauri kufahamu mapato  yaliyokusanywa na Wakala/Wakusanya mapato hao.

Vile vile, mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya benki, na hivyo kuwezesha Halmashauri kufahamu kiasi ambacho Wakala/Mkusanya mapato amekiingiza kwenye akaunti ya benki ya Halmashauri ikilinganishwa na kiasi alichokusanya. Mpaka sasa, Halmashauri zote 185 tayari zimewekewa mfumo huu wa LGRCIS.

Wakati huo huo alieleza Kuhusu Vitabu 379 vya Kukusanyia Mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi amesema  Licha ya kuwa  idadi ya Halmashauri na idadi ya vitabu vya kukusanyia mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi imepungua kutoka  871 katika Halmashauri 57 kwa mwaka 2015/16 mpaka vitabu 379 katika Halmashauri 21 kwa Mwaka 2016/17, OR – TAMISEMI imeendelea kusimamia maelekezo ya Serikali ya Halmashauri zote ziachane na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi/vitabu vya kuandikwa kwa mkono, na badala yake mapato yakusanywe kwa kutumia mashine za kielektroniki.

Waziri Jafo alimalizia kwa kutolea ufafanuzi wa Soko la Mwanjelwa –Mbeya na kusema kuwa OR-TAMISEMI imeanza kuchukua hatua kuhusiana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa na kwa kuanza tulimuomba CAG kufanya ukaguzi maalum na taarifa iliashiria makosa ya kijinai na tayari Serikali imelifikisha suala hili kwenye vyombo vya Dola, ambapo pia Wahusika Wakuu wa mikataba husika na usimamizi wa utekelezaji wake, nao pia wameshafikishwa kwenye vyombo vya Dola kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi. Serikali itaendelea kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na CAG ili kuokoa hasara itokanayo na ujenzi wa soko hilo

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate  zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: