Tuesday, 10 April 2018

Wawili Wafariki kwa Mafuriko Mwanza


Wakati mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha mafuriko,  Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja wamefariki baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha zilizokuwa na upepo mkali.

Akizungumza kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wa April 9 wakati wakiwa wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.

Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) huku majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.

No comments:

Post a comment