NA TIMOTHY ITEMBE TARIME.
WATOTO 54 wa shule za msingi zilizopo ndani ya halmashauri ya mji wilayani Tarime mkoani Mara wamedaiwa kulawitiwa kwa nyamati tofauti

Akizungumza mbele ya Madiwani wa baraza la kawaida la halmashauri ya mji wa Tarime diwani viti maalumu kata ya Bomani,Norah Kashuku (CHADEMA) alisema kuwa baraza hilo awali ndani ya baraza kma hilo walipokea taarifa kuwa kuna kundi la watoto ambao wamejipanga na kuwafanyia vitendo vya ukatili vya kuwalawiti watoto wenzao wa madarasa ya chini ndani ya shule za msingi pindi wanapokuwa wanaingia na kutoka mashuleni.

Naye diwani viti malumu kata ya Nyandoto,Tekra Johanes (CHADEMA)Alisema kuwa matukio ya vitendo hivyo baraza lake limechukua hatua za kuliundia kamati ya ufuatilaji pia na kutoa taarifa kwa mkuu wa wilaya Tarime Glorius Luoga ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

Johanes aliongeza kuwa kamati imeundwa na kuwa kinachosubiriwa ni kamati hiyo kuanza kazi pamoja na kutoa taarifa zinazoendelea juu ya vitendo hivyo.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti halmashauri ya Tarime Mjini,Bahiri  Selemani (Sauti)alitumia nafasi hiyo kulaani vitendo hivyoa pamoja na kulaani baadhi ya wazazi wanaoshabikia na kutumia nafasi hiyo kurudi kwenda kupatana na upande wa mtuhumiwa ambapo amesema kuwa kufanya hivyo ni moja ya njia inayochangia vitendo hivyo kushamiri kuwepo.

“Mimi nitumie nafasi hii kuwaasa wazazi kuacha tabia ya kuelewana na upande wa Mtuhumiwa pindi inapobainika kuwa amaekamatwa kuhusiana na vitendo vya ulawiti na ubakaji”alisema Sauti.
Selemani alitolea mfano kijaa moja aliyekematwa kutoka ndani ya mtaa wake akijihusisha na vitendo hivyo kuwa baada ya kuwa amekamatwa wazazi wa mlalamikaji walirudi kwenda kuelewana kinyumbani na upande wa mtuhumiwa jambo ambalolinakatisha jitihada za serikali katika kufuatilia na kutetea wahanga wa matukio kama hayo

Akijibu hoja hiyo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Tarime,Belton Garigo alisema kuwa swala hilo wamelipata na tayari wamekwisha lifikisha kushugulikiwa  katika ngazi husika.

Kaimu huyo aliongeza kuwa ndani ya  halmashauri yake kuna shule za msingi 30 na za  watu binafsi zipo 05 na kuwa watoto walioadhirika zaidi ni wale wanaosoma katika shule za seikali kwa sababu ya usafi  wa miguu.

“Watoto wanaoadhirika zaidi na vitendo hivyo ni wale wa  madarasa la chini hususani darasa la tatu hadi la sita ambapo wanafanyiwa na watoto wa umri mkubwa waliozoea kufanya vitendo hivyo”alisema Garigo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: