Wednesday, 18 April 2018

Watoto 20,000 Kupatiwa Chanjo ya Satani ya Shingo ya Uzazi


Zaidi ya Watoto wa kike  20,000 wenye umri wa miaka 14 watapatiwa chanjo ya saratani ya shingo ya uzazi  mkoani Arusha katika jumla vituo vya afya  372 pamoja na shule zitakazoanisha kutumika katika utoaji wa chanjo hiyo.

Mratibu wa Chanjo mkoa wa Arusha Aziz Sheshe amesema kuwa chanjo hiyo itawakinga watoto  kike na ugonjwa huo ambao husababisha maumivu makali na hata kupelekea vifo vya watoto.

Azizi amesema kuwa tayari vituo 292 viko tayari kwa kutoa huduma hiyo hivyo amewataka watoto wenye umri huo kujitokeza katika vituo hivyo ili kupata huduma bora ya chanjo inayotolewa na serikali.

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega  amesema kuwa  ni vyema jamii ikaondokana na mila potofu ambazo hujitokeza kwani chanjo hiyo ni salama na itakoa maisha ya watoto wa kike wanaopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa saratanii  ya  shingo ya uzazi na matiti husababisha karibu asilimia 50% ya vifo vyote.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Timoth Wonanji amesema kuwa  chanjo hiyo ni juhudi za serikali na wa maendeleo katika kupambana na saratani ya mlango wa uzazi ambayo inakua kwa kasi hivyo juhudi hizo zitasaidia kupunguza ama kutokomeza  ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo  na Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro wamesema kuwa chanjo hiyo ni mkombozi  wa watoto wa kike katika taifa la Tanzania hivyo amewataka Watoto wa kike kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata kinga inayotokana na chanjo hiyo.

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 

No comments:

Post a comment