Watatu kati ya Sita waliotekwa na wasiojulikana waonekana


WATU watatu kati ya sita waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha usiku wa kuamkia Ijumaa,  Aprili 6, 2018 katika Kijiji cha Mitambuuni shehia ya Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba wameonekana alfajiri ya leo Jumapili Aprili 8, 2018  katika Kijiji cha Mkungu Jimbo la Mtambile wilayani Mkoani.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Sheikhan Mohamed Sheikhan, amethibitisha kupatikana kwa watu  hao ambao ni vijana, kuwa ni Said Shanani Mohamed (16),  Juma Kombo Fimbo (17) na Abdallah Khamis Abdallah (19).
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: