Monday, 9 April 2018

Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba


Na Agness Francis

Wasanii wa nyanja zote  wakumbushwa kuzingatia na kuwa makini kuzitambua aina 7 za sheria katika zoezi zima la kusaini mikataba mbalimbali katika kazi zao hapa Nchini.

Akizungumza na wasanii mbalimbali  leo katika ukumbi wa Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) Jijini Dar es Salaam Wakili wa kampuni ya Setla,  Noeli Chikwindo amesema kuwa ni vema kwa wasanii kufahamu sheria 7 za usaini wa mikataba ili kupata haki zao zinazostahiki.

" Ni vema kabla hujatia saini  ufahamu ni kitu gani unasaini pamoja na kuelewa vizuri  lugha iliyotumika katika mkataba huo ili kuepuka matatizo ya baade yatakayojitokeza"amesema wakili Chikwito.

Vile vile amewataka wasanii kuwa makini na kazi zao pindi wanapoingia mkataba na kampuni yoyote kuzingatia zile sheria 7 katika makubaliano hayo.

"Msanii ni muhimu kufahamu  masharti ya mkataba kabla ya makubaliano inasaidia kuepuka usumbufu wa kupata haki yako,na wakati mwinginine msanii hulalamika kumbe yeye ndo chanzo cha matatizo" amesema wakili Chikwindo.

Aidha msanii wa muziki wa dansi  Franswaa Makasi  amewataka wasanii wenzake wa nyanja mbalimbali wajitambue katika kuzingatia  mikataba wanayosaini kuwa na vipengele vyote  vya sheria ili kuondokana na usumbufu

"Wasanii wenzangu ifike mahari tujitambue  ili haki zetu zipate kutendeka sawa,kazi zipo mikataba ipo lakini hatujitambui na sisi tutende haki  upande wa pili maana wasanii wengine vile vile hawatendi haki" amesema makasi Junior.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: