Monday, 9 April 2018

Wanawake waliotelekezwa na waume zao DAR watema cheche mbele ya RC Makonda


Leo Jumatatu Aprili 09, 2018 Mamia ya wanawake waliotelekezwa na waume jijini Dar es salaam wamefurika kwenye ofisi za mkuu wa mkoa, Paul Makonda kufuatilia masuala ya sheria kama mkuu huyo wa mkoa alipoagiza awali Machi 22, 2018

Wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi, wanawake hao wamesema kuwa wanajisikia uchungu kutelekezwa na waume zao kwani jukumu la kulea watoto ni jukumu la wazazi wote wawili.
Kwa upande mwingine wanawake hao wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo hicho cha kuwasaidia na wamemtakia maisha marefu kwani tatizo hilo ni kubwa kwenye jamii.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: