Saturday, 21 April 2018

Wanaume Waliokaidi Wito Wa Rc Makonda Kukamatwa Jumatatu


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema wanaume wote waliokaidi wito wa kufika ofsini kwake baada ya kupigiwa simu na kutumiwa barua za wito watakamatwa na Jeshi la Polisi kuanzia siku ya jumatatu ya April 23.
 
RC Makonda amesema ifikapo siku ya Jumapili majina ya wanaume waliokaidi wito yatafikishwa kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Benedict Mambosasa kwaajili ya utekelezaji.
 
Aidha RC Makonda ameongeza siku nyingine tano kwaajili ya kusikiliza kesi zilizowasilishwa ofisini kwake na kufanya idadi ya kufikia siku 15.
 
Pamoja na hayo RC Makonda amesema ataunda kamati ya wanasheria na maafisa ustawi wa jamii kutoka serikalini na taasisi binafsi kwaajili ya kufanya uchambuzi wa ukubwa wa tatizo na mapendekezo ya kisheria kisha kuwasilishwa wizara husika kisha kuwasilishwa Bungeni.
 
Hata hivyo RC Makonda amesema ifikapo April 25 na 26 atatoa ripoti ya mwelekeo dhidi ya mateso waliyokuwa wakipata kinamama na watoto waliotelwkezwa. 
 
RC Makonda amesema Zoezi la kusikiliza kinamama waliotelekezwa limekuwa na mafanikio makubwa ambapo zaidi ya wananchi 17,000 walifika ofsini kwake ambapo hadi sasa kinamama 7,000 wamesikilizwa na wanaume 1,200 wamekubali kwa maandishi kutunza watoto wao na wengine wamepimwa DNA.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: