Wednesday, 25 April 2018

WANASAYANSI : MAKABURI YA TILES SIYO SALAMA


Imeelezwa kwamba matumizi ya maru maru (tiles, marble , terrazzo) kujengengea makaburi sio salama kwa ardhi, kwani yana kemikali ambayo inaathiri udongo.

Taarifa hiyo imetolewa na mtaalamu wa sayansi ya mazingira na kilimo, Prof. Julius Zake wa Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, kwenye ripoti yake ya udongo wa Uganda na njia sahihi ya kutumia mbolea, na kueleza kwamba ujenzi wa makaburi kwa tiles unaongeza hatari kubwa ya udongo kushindwa kuzalisha.

“Zamani watu walikuwa wanatumia nguo maalum (backcloth ) kuzikia wapendwa wao, sasa hivi watu wanakufa sana na wanazikwa kila mahali kwa wingi,tiles haziwezi kuharibika zinaingiliana na mizizi inayorutubisha udongo na kusaidia uzalishaji, hivyo udongo unaathirika na kemikali”, amesema mwanasayansi huyo.

Mtaalamu huyo amesema ardhi sasa hivi imekuwa na acid nyingi na kusabaisha kushindwa kuwa na rutuba, ya kuweza kustawisha mazao na kutunza mazingira

No comments:

Post a Comment