Na Clonel Mwegendao
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa  na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga imeanza zoezi la kuonyesha Mipaka ya Hifadhi ya Serengeti na Wananchi katika Kata ya Kwihancha na Nyanungu ili kupunguza Migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza baina ya waifadhi na Wanachi pale Mifugo inapoingizwa kwenye hifadhi.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiambatana na Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji pamoja na Madiwani wa kata huska  ili kutambua Mipata hiyo kwa lengo la kutoa Elimu kwa Wanachi ili kuondokana na shughuli za kibinadamu kuanzia Mita Miatano kutoka kwenye Mipaka hiyo.

Lameck Emanuel ni Mhifadhi Msimamizi kanda ya Kaskazin wa hifdhi ya Serengeti pia inayopakana na Tarime amesema kuwa Maeneo ambayo yametengwa kisheria yanapaswa kukaa wazi ili kuondoa Migogoro baina yao na Wananchi huku wakiondokana suala la kuziba njia na Mawe ili magari yasipite kuwakamata majangiri wanaoingia wanaoingia katika hifadhi hiyo jambo ambao ni hatari endapo wanyama wakali watavamia Wanachi watashindwa kupita kwa sababu njia zinazibwa na Mawe.

Mustapha Masian ni diwani wa kata ya Kwihancha na Muesi Nyangombe ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyagasese kijiji Nyabirongo wameweza kuzungumzia juu ya zoezi hilo la kubaini Mipaka na kupima Mita Miatano kutoka katika Mipaka ya Hifadhi ya Serengeti  ikiwa na lengo la  kuwasaidia wananchi kuchukua tahadhari Pindo wafikapo eneo hilo ili kuepuka kushambuliwa na wanyama wakali
Share To:

msumbanews

Post A Comment: