Wednesday, 11 April 2018

WANANCHI WAKOSA MAKAZI KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA -ArushaNa  Msumba Blog
Wananchi wa kata ya Kiranyi na Ngarenaro wamekosa makazi kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia leo hivyo wameiomba serikali iwasaidie wapate makazi ya muda.

Wananchi hao  Saumu Mshana na Asia Mohamed wamesema kuwa wamepata adha kubwa wakiwemo wa kinamama wajawazito waliokua wakijitaidi kuokoa mali zao pamoja na watoto wao.
Diwani wa Kata ya Kiranyi John Seneu amesema kuwa kwa sasa kuna idadi kubwa ya watu wasiokua na makazi hivyo ameiomba serikali iweke utaratibu mzuri kwa ajili ya watu hao ili waweze kuhudumia familia zao kwa chakula na mavazi.

Katibu Tawala ya Wilaya ya Meru Timotheo Mnzava  amewataka Wakazi wanoishi kwenye maeneo hatarishi kuhakikisha kuwa wanahama na kupisha mkondo wa maji ili kuepuka madhara yanayosababishwa na mvua hizo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: