Friday, 20 April 2018

WAMILIKI WA ARDHI WANAOKWEPA KODI KUFUTIWA HATI
Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Afisa Ardhi Mwandamizi  kanda ya Kaskazini  Thadeus Riziki  amesema kuwa Wizara ya Ardhi haitasita kuwafutia hati wamiliki wa ardhi ambao hawalipi kodi ya ardhi  hivyo kupoteza umiliki wa maeneo yao kisheria hivyo amewataka wamiliki hao kulipa kodi kwa wakati ili nja vya wasipoteze umiliki wa ardhi zao.

Thadeus ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa wanachi katika viwanja vya stendi ya kilombero jijini Arusha ambapo amesema kuwa wizara imetoa muda mwisho ni April 30 mwaka huu watakaokaidi agizo hilo watapelekwa mahakamani na kuchukuliwa hatua ikiwemo kufutiwa umiliki wa ardhi zao.

Amewataka Wananchi kulipa kodi hiyo ya ardhi kwa serikali kuu pekee ambayo pia inalipwa kwa simu ya kiganjani na wanaweza kupata maelezo juu ya viwanja vyao katika tovuti ya wizara ya ardhi.

“Waziri lukuvi aliongeza muda kwa matumaini kuwa wamiliki wataitikia wito wa kulipa kodi hivyo hivyo ni vyema wananchi wakaitumia fursa hiyo mapema” Alisema Afisa huyo

Wakazi wa Arusha Godlisten Shayo na Saumu Ally wamesema kuwa elimu juu ya ulipaji kodi inapaswa kutolewa mara kwa mara ili kujenga utamaduni wa kulipa kodi bila shurti.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: