Friday, 20 April 2018

Walichokiamua wasanii Bongo Movie Usiku Huu Kuhusu Mazishi ya Agness Masogange


Wasanii mbalimbali wa filamu na wa bongo fleva, wamekutana katika viwanja vya Leaders Club usiku huu  ili kujadiliana kuhusu utaratibu wa mazishi ya msanii anayepamba video za muziki (video queen), Agness Gerald maarufu Masogange.

Steve Nyerere amesema kuwa, Masogange anatarajiwa kuzikwa Mbeya na kuwa mwili utasafirishwa Jumapili wiki hii na kuzikwa Jumatatu.

Miongoni mwa wasanii waliofika Leaders leo ni pamoja na Chopa wa Mchopanga, Irene Uwoya aliyeambatana na mume wake, Dogo Janja na aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media Group, Zamaradi Mketema.

Kamati ya awali iliyoundwa, imemchangua Mchopanga kuwa katibu na Zamaradi kukusanya michango.

“Lakini tukipata taarifa kutoka kwa ndugu tutajua msiba utagharimu shilingi ngapi kwa sasa mahitaji makubwa ni mabasi mawili kwa ajili ya kusafirisha mwili, maturubai, vyakula na maji,” amesema Nyerere.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: