Wabunge wa wametakiwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Ushauri huo umetolewa mara baada ya kufanyika utafiti uliofanywa na shirika la 'Action On Disability and Development' kwa kushirikiana na shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania kubaini kuwepo kwa vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto wenye ulemavu.

Akiongea na Wabunge katika semina iliyoandaliwa na Shirika la ADD, Mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Rose Tesha amesema kuwa baadhi ya ndugu na jamaa wamekuwa wakishiriki vitendo hivyo hususani kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na akili.

Wakitoa maoni yao katika Semina hiyo baadhi ya wabunge wametaka sheria iweze kurekebishwa ili mfuko wa jimbo pia uweze kuwahudumia watu wenye ulemavu huku wengine wakitaka uboreshaji wa miundombinu kwa watu wenye ulemavu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: