Tuesday, 24 April 2018

VITA YA MABINGWA ULAYA, NI LIVERPOOL DHIDI YA ROMA LEOVita ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea tena usiku wa leo ambapo Liverpool watakuwa wanaikaribisha AS Roma kwenye Dimba la Anfield.

Liverpool waliingia hatua ya nusu fainali baada ya kuing'oa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1 huku nyota wake Mohamed Salah aking'aa.

AS Roma nao walitinga hatua hiyo kufuatia kupindua matokeo dhidi ya vinara wa ligi nchini Spain, FC. Barcelona.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka duniani, itaanza majira ya saa 3 na dakika 45 za usiku.

Baada ta mtanange huo, kesho pia ligi hiyo itaendelea kesho kwa Bayern Munich kuikaribisha Real Madrid kutoka Spain.

No comments:

Post a Comment