Mjumbe wa Kamati Kuu, na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Sheria ya ACT Wazalendo, Wakili Thomas Msasa amekamatwa na polisi mjini Kigoma.

Tarifa ya kukamatwa kwake imetolewa na Mbunge wa Kigoma Ujiji Zitto Kabwe, na kusema kwamba sababu ya kukamatwa ni  kuwatetea Madiwani, viongozi na wanachama wa chama hicho waliokuwa wamekamatwa na Jeshi la Polisi hapo jana.

Zitto Kabwe amesema wakili Msasa alikwenda polisi kama wakili wa Madiwani wawili wa ACT Wazalendo, diwani wa kata ya Kipampa, ndugu Mussa Mgongolwa, pamoja na diwani wa kata ya Kigoma, ndugu Hussein Kalyango, aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Mwanga, ndugu Winston Mogha, katibu wa ngome ya vijana ya ACT Wazalendo mkoa, ndugu Masabo, pamoja na wanachama na wafuasi mbalimbali wa ACT Wazalendo wa mkoa wa Kigoma, ambao walikamatwa hapo jana.

Kwa upande wa msemaji wa chama hiko Ado Shaibu amesema mpaka sasa upande wa jeshi la Polisi hawajatoa taarifa rasmi juu ya sababu ya kukamatwa kwa watu hao, na kwamba wanasheria wao wanashughulikia suala hilo na utaratibu wa dhamana.

Isome hapa taarifa yote aliyoandika Zitto Kabwe.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: