Wednesday, 25 April 2018

Ulaya yapiga marufuku watoto wa chini ya miaka 16 kutumia WhatsApp

Wamiliki wa mtandao wa message wa WhatsApp wametangaza kufungia watoto wa umri wa chini ya miaka 16 kutumia mtandao huo katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU).

Kwa sasa mtumiaji anapaswa kuwa na umri wa angalau miaka 13, jambo ambalo linabadilishwa kupitia miongozo mipya ya usiri wa data katika nchi hizo kuanzia mwezi May.

Inaelezwa kuwa App hiyo ambayo inamilikiwa na Facebook, itahitaji mtumiaji kueleza ana umri gani pindi anapoanza kuitumia kuanzia wiki chache zijazo.

Watoto wa miaka 14 na 15 waoana kwa idhini ya mahakama ya dini

 Inaripotiwa kwamba theluthi ya watoto wote wa kati ya umri wa miaka 12 na 15 wanaoishi nchini Uingereza ambao wanatumia mitandao ya kijamii pia wanatumia WhatsApp

No comments:

Post a Comment