Wednesday, 4 April 2018

Ujauzito wa Zamaradi wazua gumzo

Zamaradi Mketema

MIMBA ya mtangazaji maarufu wa TV, Zamaradi Mketema usiku wa Aprili Mosi ilizua gumzo katika ukumbini kutokana na kwamba, hapo awali hajawahi kubambwa akiwa na tumbo.

Zamaradi alionekana akiwa na ujauzito mkubwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani City kulikokuwa na zoezi la utoaji Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu (SZIFF) hali iliyozua gumzo kwa watu waliohudhuria kwenye tukio hilo.

Gumzo lilizidi zaidi baada ya Zamaradi kuitwa jukwaani kwa ajili ya kukabidhi tuzo kwa mshindi katika kipengele cha Muongozaji Bora ambapo alimtangaza mshindi Daniel Manege aliyeshinda kupitia filamu ya Safari ya Gwalu.

“Si juzijuzi tu kaolewa mara hii tayari ana mimba? Ona gauni lake lilivyombana, tumbo lote linaonekana wakati alikuwa akifanya siri kwani hata kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii amekuwa akiweka picha za uso tu,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji ukumbini hapo akijadiliana na mwenzake.

Zamaradi aliyewika na Kipindi cha Filamu cha Take One akiwa Clouds, aliolewa ndoa ya kimyakimya Septemba, mwaka jana ambapo kabla ya hapo alikuwa na watoto wawili aliozaa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: