Monday, 9 April 2018

Uhamiaji yafafanua sababu za kudai vyeti vya kuzaliwa Vya Wazazi wa Nondo


Idara ya Uhamiaji imesema Watanzania wote waliozaliwa kuanzia mwaka 1978 wanapaswa kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Crispin Ngonyani amesema hayo leo Jumatatu Aprili 9, 2018 alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Ngonyani amesema hayo alipotoa ufafanuzi kuhusu maagizo yaliyotolewa na Uhamiaji kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo ya kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake, babu na bibi zake linavyoweza kutekelezwa.

"Tulimweleza Nondo na mwanasheria wake kuwa, kama hawana vyeti vya kuzaliwa wanaweza kuleta affidavit (hati ya kiapo) na hilo tulikubaliana," amesema Ngonyani.

Amesema, "Lakini kama mtu umezaliwa kuanzia mwaka 1978 kwa sheria yetu lazima uwe na cheti cha kuzaliwa na tukikuomba utapaswa kutuonyesha kwa hiyo wananchi wanapaswa kulijua hili."

Nondo ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) alihojiwa Aprili 5, 2018 kuhusu uraia wake na ametakiwa kupeleka vielelezo kuthibitisha uraia wake vikiwamo vyeti vya wazazi, bibi na babu wa pande zote

No comments:

Post a comment