Tundu Lissu Apasuliwa tena Mguu - MSUMBA NEWS BLOG

Tuesday, 10 April 2018

Tundu Lissu Apasuliwa tena Mguu

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili 11, 2018 ataingia kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.

Lissu ambaye ameshafanyiwa upasuaji mara kadaa katika Hospitali ya Nairobi nchini kenya kisha Ubelgiji, amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu. 

==>>Hii ni Kauli yake 

Habari za leo popote mlipo wapendwa wangu. .
Napenda kuwajulisha kwamba ndani ya nusu saa ijayo ninaingia kwenye operesheni nyingine tena. .

Kama nilivyowataarifu siku za nyuma, mguu wa kulia bado una shida kutokana na risasi nyingi nilizopigwa na 'watu wasiojulikana.' Operesheni ya leo ni sehemu ya tiba ya mguu huo. .

Napenda wote mfahamu kwamba niko kwenye mikono salama ya kitabibu. .

Mungu wetu amekuwa mwema sana kwangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana. Na hili pia litapita. .

Wasalaam.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done