Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imepata pigo kubwa baada ya watumishi wake watatu kuacha kazi kwa mpigo, huku wakilaumu uongozi wa Tume hiyo
Wafanyakazi hao ambao ni Kaimu Mwenyekiti Consolata Nkatha Maina, Kamishna Margaret Mwachanya na Paul Kurgat wamejiuzulu wadhifa wao na nafasi zao za kazi ndani ya tume hiyo, huku wakisema kwamba Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameshindwa kuongoza.
“Kwa muda mrefu sana na mara nyingi mno, mwenyekiti wa tume ameshindwa kuwa na mkono thabiti na imara, badala yake chini ya uongozi wa Chebukati, bodi ya tume imekuwa mahali pa kutembea kwa habari zisizo za ukweli, misingi ya kutokuaminiana na kujitafutia sifa binafsi. Taasisi imesababishwa kutoweza kufanya uamuzi, kuvuja nyaraka za ndani ili kutumikia malengo binafsi na kufuata maslahi binafsi, yote ambayo ni kinyume na sheria iliyowekwa ambayo inasimamia mwenendo wa uongozi wa tume na wafanyakazi”, wamesema wafanyakazi hao ambao miongoni mwao yumo Kaimu Mwenyekiti wa Tume.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amempa likizo ya lazima Mkurugenzi wa Tume Ezra Chiloba bila sababu maalum, huku wengi wakilaumu kitendo hicho, wakisema kuwa Chebukati anaendesha Tume kwa maslahi yake binafsi.
IEBC imekuwa ikilaumiwa kwa matukeo ya uchaguzi wa mwaka 2017 wa viongozi wa Kenya, ambao pia ulisababisha kufutwa kwa matokeo ya Urais, kwa uchaguzi wa Agosti 8, 2017.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: