TFF yamtangaza mchezaji bora


Mchezaji wa timu ya Lipuli yenye maskani yake mkoani Iringa, Adam Salamba amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) kwa mwezi Machi.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) alasiri ya leo Aprili 13, 2018 na kusema Salamba ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake wawili ambao ni Salum Kimenya wa Prisons na kipa wa Azam, Mwadini Ally.

TFF imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kufanyika uchambuzi na Kamati ya Tuzo iliyochaguliwa na shirikisho na hatimaye kumpata mshindi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: