Ile rufaa inayomhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Richard Wambura, imesikilizwa jana kwa pande zote mbili kukutana katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala.

Kwa mujibu wa Wakili wa Wambura,Emmanuel Muga, amesema pande zote mbili zimemaliza vizuri kikao hicho na mambo yamekwenda sawia, kinachosubiriwa tu sasa ni maamuzi ya Kamati ya Maadili kutoa hukumu.

Muga ambaye anamtetea Wambura, ameeleza TFF wamesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo.

Wambura alikata rufaa kupinga kufungiwa kujihusisha na soka baada ya TFF kumfungia kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.

Kamati ya Maadili itakaa na kuandaa rasmi na majibu ya hukumu juu ya rufaa hiyo iliyosikilizwa jana Jumamosi.q
Share To:

msumbanews

Post A Comment: