Mhifadhi wa Tembo, Daphne Sheldrick kutoka nchini Kenya amefariki dunia kwa maradhi ya saratani akiwa na umri wa miaka 83, jana April 13, 2018.

Daphne alisaidia kuokoa maisha ya tembo zaidi ya 230 wengi wao ambao walipoteza mama zao kwa ujangili au ukame kwa kutengeneza mpango maalumu wa kuwapatia maziwa na kufanikiwa kwa ufanisi.
Mama huyo alizaliwa na kukulia nchini Kenya, alitumia takribani nusu ya miaka yake ya kwanza kazini, akifanya kazi pamoja na mume wake ambaye alikuwa Mwingereza David, ambaye ndiye aliyegundua Hifadhi ya Taifa Tsavo Mashariki nchini Kenya.
Baada ya kifo cha mumewe mwaka wa 1977, alianzisha mfuko wa David Sheldrick Wildlife Trust (DSWT), ambao unajulikana zaidi kwa kuokoa na kuimarisha tembo yatima porini.

Ilimchukua miaka yake 28 kufanikiwa kutengeneza formula maalum ya kunyonyesha tembo kwa maziwa ya chupa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: