Friday, 20 April 2018

TAKUKURU imewafikisha mahakamani waliokuwa viongozi NCU

Na James Timber, Mwanza
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, inawafikisha mahakamani leo waliokuwa viongozi waandamizi wa Shirika Nyanza Cooperative Union (NCU), kwa tuhuma za ubadhirifu na ufujaji wa mali.

Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Susan Mwendi amesema, uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU kuwa aliyekuwa  Mwenyekiti Jacob Shibiliti na Makamu wake John Magulu ilibainika kati ya Januari 1, 2003 hadi Desemba 31, 2004  waliisababishia hasara NCU jumla ya Tshs.426,400,000 kwa kipindi hicho huku Makamu Mwenyekiti aliisababishia hasara shirika hilo takribani Tshs.332,640,000.

Mwendi amesema kuwa watuhumia waliisababishia NCU, hasara kinyume na Aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza pamoja na kifungu cha 57(1) na 60(2) vya sheria ya Uhujumi uchumi, sura ya 200 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

"Watuhumiwa waliuza mali ya  NCU kinyume na taratibu viwanja vya Kitalu B eneo la viwanda Kata ya Igogo kwa Kampuni ya VICKFISH Ltd kwa Tshs.20,000,000/- bila kufanya uthaminishaji huku thamani ya viwanja hivyo kwa kipindi hicho ilikuwa Tshs.426,400,000/- na kuridhia uuzwaji wa viwanja hivyo kwa Tshs.20,000,000," amesema Mwendi.

Pia iligundulika Mwenyekiti John Magulu alisaini kwa niaba ya NCU mkataba wa kuuza Kiwanda cha Mkonge, plot Na.41 a na 79 Mwanza South kwa gharama ya Tshs. 123,000,000/- ili kulipa deni Tshs. 1,942,543,000/-  waliokuwa wanadaiwa na benki ya NBC.

Pia kiwanda hicho cha Mkonge katika Plot Na. 41 na 79 Mwanza South kwa mwaka 2001 vilikuwa na thamani ya Tshs.444,640,000 ambapo kikauzwa kwa Tshs.123,000,000 na kuhisababishia hasara NCU ya Tshs.332,640,000.

Aidha Kamanda ametoa rai kwa wananchi kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja, kuomba na kupokea rushwa ni kosa la jinai, kila mmoja awajibike kukemea vitendo vya rushwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: