Thursday, 12 April 2018

Spika Abadili Mlango kwa sababu za kiusalama

Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameonyesha utaratibu mpya wa kuingia bungeni tofauti na ilivyokuwa awali.
Spika Ndugai ametoa utaratibu huo wakati akiingia bungeni ambapo amesema kuwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge wataingia bungeni kwa kutumia mlango mdogo unaoelekea kwenye chumba maalumu cha spika kwasababu za kiusalama.
“Waheshimiwa Wabunge kwakuwa tumekuwa tukifanya kwa kuiga wenzetu tutaanza kutumia utaratibu mpya tulionza kuingia leo, kwa msafala wa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kuingia na kutoka Bungeni kwakutumia mlango wa kuelekea kwa speakers lounge.Waheshimiwa Wabunge mlango mkuu wa mbele utaendelea kutumika na Waheshimiwa Wabunge kama kawaida yenu na Spika na Msafara wake atautumia mlango huu mkuu wakati wa matukio maalum ya Kibunge kama vile wakati wakufunga na kufungua Bunge au tukiwa na ugeni wa Kitaifa kama Mh. Rais akitutembelea tutaingia kwa lango lile Kuu katika siku za kawaida tutatumia mhuu utaratibu niliyoutumia leo,” alisema Spika.
“Kwahiyo hiyo ndio taarifa niliyokuwa nataka kuitoa na ina faida nyingi wakati mwingine mnaweza mkawa na hasira tukapita hapa mkaturukia hapa katikati ikawa tabu kwahiyo hata kiusalama hapa ni bora zaidi.”

No comments:

Post a comment