Wednesday, 18 April 2018

SIMBA YATUA MOROGORO KUANZA MAWINDO DHIDI YA LIPULI


Kikosi cha Simba kimewasili mjini Morogoro mchana huu kwa ajili ya kambi ya muda mfupi kabla ya kuelekea Iringa kukipiga na Lipuli FC katika mchezo wa ligi kuu.

Simba imeondoka jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons iliyoupata Jumatatu ya wiki hii.

Wekundu wa Msimbazi watakuwa mjini hapo kwa siku kadhaa wakifanya mazoezi kisha Ujumaa watanzaa safari ya kuelekea Iringa.

Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Samora kuanzia majira ya saa kumi kamili jioni.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: