Saturday, 14 April 2018

Simba yaanza kujinoa dhidi ya Tanzania Prison
Baada ya kupewa mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi jioni hii katika Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Simba itakuwa mwenyeji dhidi ya Prisons Jumatatu ya Aprili 16 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinafanya mazoezi hayo baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City FC kwa jumla ya mabao 3-0.

Simba wako kileleni mwa msimamo wa ligi hivi sasa wakiwa na alama 55 kibindoni, huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 47.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: