Monday, 9 April 2018

Simba waimaliza Mtibwa

Klabu ya simba imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Mtibwa Sugar ugenini mkoani Morogoro mchezo uliyopigwa dimba la Jamhuri
Bao la Simba limepatikana dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake hatari raia wa Uganda, Emmanuel Okwi.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 52 dhidi ya 46 za hasimu wake Yanga SC ambao wana mchezo mmoja mkononi.
Klabu ya Simba inahaha kuhakikisha inatwaa ubingwa huo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kulikosa kwa miaka mitano mpaka sasa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: