Thursday, 19 April 2018

Simba wafanya mazoezi Morogoro Leo kwa maandalizi dhidi ya Lipuli


Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi yake leo kikiwa mjini Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wake wa ligi dhidi ya Lipuli FC.

Simba imeweka kambi maalum ya muda mfupi mjini Morogoro kabla ya kuondoka kesho Ijumaa kuelekea Iringa kukipiga na Lipuli.

Wekundu hao wa Msimbazi waliwasili jana majira ya saa 7 mjini Morogoro ili kuanza kujinoa kwa ajili ya safari ya kuwania ubingwa uliokosekana kwa takribani misimu mitano.

Kikosi hicho kinahitaji jumla ya alama 14 pekee ili kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi msimu huu, na hivi sasa wapo mbele kwa jumla ya utofauti wa pointi 11 dhidi ya Yanga.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: