Simba SC kuchuana na Mbeya City Leo


Kikosi cha Simba kinaendeleza safari yake ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu kitakapowakaribisha Mbeya City FC katika Uwanja wa Taifa leo.

Simba inaingia kibaruania ikiwa juu ya msimamo wa ligi kwa kujikusanyia alama 52 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga walio nyuma kwa alama 5 wakiwa na pointi 47.

Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili Uwanja wa Taifa huku Simba ikiongezwa nguvu na wachezaji wake Juuko Murushid, Erasto Nyoni na James Kotei kurudi kikosini baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Tayari timu zote mbili zimeshakamilisha maandalizi hayo jana kuelekea mchezo huo utakaopigwa jioni hii.

Ushindi wa Simba leo utazidi kupeleka machungu kwa Yanga maana itaongeza utofauti wa lama kutoka 5 mpaka nane.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: