Tuesday, 1 May 2018

SIMBA KUANZA MAANDALIZI DHIDI YA NDANDAKikosi cha Simba kinatarajia tena kambini kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.

Simba itakuwa inashuka kucheza na Ndanda Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kuwa kikosi kimepewa mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kurejea kambini kwa ajili ya Ndanda.

Wekundu hao wa Msimbazi watakuwa wanarejea kambini wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliopita

No comments:

Post a Comment