MSANII wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa siku akitibuka atampeleka moja kwa moja mzazi mwenzie Dickson Matoke kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa ajili ya kudai haki ya kuhudumiwa mtoto wake.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa sio kwamba hana uwezo wa kumhudumia mtoto wake lakini kuna wakati unaumia kuona baba wa mtoto yupo, anakula bata tu akiwa hajui hata kula ya mtoto wake inatoka wapi.

“Dawa ya wanaume wa sampuli hii ni kuwapeleka tu kwa Makonda. Mimi watu watashangaa sana siku watakaponiona pale lakini ni kwa sababu wakati mwingine ukifikiria unajikuta unapatwa na hasira kuona mzazi yupo lakini kama hayupo vile,” alisema Shamsa.

Tangu Jumatatu iliyopita, akinamama wengi waliotelekezewa watoto wamekuwa wakifika kwa Makonda ili kusaidiwa lakini hakuna staa wa kike aliyetinga hadi juzi Alhamis.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: