Wafanyakazi wa uokoaji pamoja na madaktari walioko katika eneo la Mashariki mwa Ghouta nchini Syria, wamethibitisha kuwa watu zaidi ya 100 wameuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika shambulio baya la Kemikali.

Hata hivyo Serikali ya Rais Bashar Al- Asaad wa Syria imekanusha kutumia kemikali hiyo ya sumu dhidi ya raia.

Idara ya kimataifa ya usalama nchini Marekani, inasema kuwa, inafuatilia kwa karibu mno taarifa zinazohuzunisha za matumizi ya silaha za kemikali Wilayani Ghouta Mashariki.

Shambulio linaloashukiwa kuwa la kigaidi, lililolenga mji wa Douma, eneo linaloshikiliwa na waasi Mashariki mwa mji wa Ghouta, limetokea baada ya majuma kadhaa ya milipuko ya mabomu kutoka angani, iliyotekelezwa na wanajeshi wa Syria.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: