Tuesday, 10 April 2018

Serikali yaeleza mpango wa takwimu kwa walemavuSerikali kupitia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu), Stella Ikupa imesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa Takwimu kwa watu wenye ulemavu.

Ikupa ameyasema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge Khadija Nasri Ally alieuliza
Kutokuwa na Takwimu kwa watu wenye ulemavu inapelekea kushindwa kuwapatia mahitaji yao ipasavyo, Je ni lini serikali itaona umuhimu wa kufanya takwimu ili kupata idadi kamili ya watu wenye ulemavu?
“Kwa niaba ya Waziri Mkuu serikali inatambua umuhimu wa Takwimu kwa watu wenye ulemavu na sambamba na hilo kama tunavyofahamu sensa huwa inafanyika kila baada ya miaka 10 kutokana na kwamba ilifanyika mwaka 2012 kwahiyo tuanategemea sensa nyingine ifanyike mwaka 2022 lakini kwasababu ya umuhimu wa jambo hili yaani takwimu kwa watu wenye ulemavu tayari serikali imeshaanza kufanya mazungumzoya kuangalia ni kiasi gani tunaweza kufanya takwimu hizi kabla ya huo wakati,“ amesema Ikupa.
“Hili suala serikali imeliangalia kwa umuhimu wake kabisa kwasababu ni makusudi na nia ya serikali kuona kwamba inapanga bajeti zake kulingana na mahitaji ya watu wenye ulemavu.“
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: